BC Banner New

Katika kuendelea na utekelezaji wa mkakati huo, Chuo cha Bandari Dar es Salaam kimepokea ugeni kutoka Chuo cha APEC kilicho chini ya Bandari ya Antwerp ya nchini Ubelgiji na Umoja wa Ulaya (EU) kwa ajili ya majadiliano ya kushirikiana katika kujenga uwezo kwa wafanyakazi.

Ugeni huo umepokelewa na Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Tafiti na Ushauri wa Kitaalam Eng. Dkt. Ramadhani Kivugo, kwa niaba ya Mkuu wa Chuo cha Bandari Dkt Lufunyo Hussein.

Ugeni huo ulitembelea maeneo mbali ya chuo ili kujionea jinsi chuo kinavyoendesha shughuli zake ikiwemo mafunzo mbalimbali ya muda mrefu na muda mfupi.

BC Antwerp Partnership4

Ugeni ulipata nafasi kutembelea na kujionea vifaa mbalimbali vya kusaidia kwenye utoaji mafunzo kama “Equipment Training Simulators”, maabara ya komputa na maktaba ya chuo. Aidha, ugeni huo ulipata nafasi ya kupatiwa wasilisho linaloonyesha utekelezaji wa shughuli za chuo kwa sasa, ikiwa ni pamoja na mpango wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania wa uendelezaji wa chuo cha Bandari Dar es Salaam.

BC Antwerp Partnership

 

Katika uendelezaji na uboreshaji wa miundombinu ya chuo na ufundishaji, TPA kupitia chuo cha Bandari Dar es Salaam itawekeza kwenye mradi mkubwa wa majengo mapya ya kisasa na vifaa vya kisasa vya ufundishaji, kufanya tafiti na kutoa ushauri wa kitaalam kwa kampasi kuu Tandika na kampasi ya kurasini Dar es Salaam. Katika majumuisho ya ziara ya ugeni huo, Taasisi hizi zimekubaliana kushirikiana katika uendelezaji na ujengeaji uwezo kwa wafanyakazi wa chuo ili kutekeleza majukumu yao ya kuzalisha rasilimali watu wenye uwezo na vigezo kulingana na hitajio la soko na wawekezaji katika sekta, kufanya tafiti tumizi mbalimbali ambazo zitajibu changamoto mbalimbali za mamlaka na sekta kwa ujumla, na kutoa ushauri wa kitaalam ili kuongeza ufanisi wa uendeshaji na usimamizi wa shughuli za Bandari Tanzania.

 BC Antwerp Partnership2

 

BC Antwerp Partnership3